Follow us

Responsive Advertisement
Responsive Advertisement
Bilionea wa Simba, Mohammed Dewji (pichani chini), amewafanyia bonge la sapraizi wachezaji na mabosi wa klabu hiyo akiwakutanisha na watu mashuhuri wakati wa tuzo maalumo za ‘MO Simba Awards 2018’.
Katika sapraizi yake hiyo ya utoaji wa tuzo zitakazotolewa keshokutwa Jumatatu jijini Dar es Salaam, hafla hiyo inaweza kuwa mwanzo wa utajiri wa Simba.
Dewji, ambaye amekuwa hafanyi masihara kumwaga fedha pindi linapokuja suala la kutaka Simba ifanye vizuri, amepanga kuwakusanya vigogo 60 wanaoongoza makampuni makubwa mbalimbali ndani na nje ya nchi ambao watashiriki katika hafla hiyo inayotarajiwa kuandika historia ya kipekee.
Ingawa mabilionea hao wataalikwa kama marafiki wa karibu wa tajiri huyo anayewanyima raha Yanga kwa sasa, lakini inaielezwa wanaweza kufunguliwa milango ya kuanza kumwaga fedha ndani ya klabu hiyo ambayo, imepania kufanya mambo makubwa baada ya kubadili muundo wake wa uendeshaji.
“Ni hafla itakayohudhuriwa na watu wasiozidi 200, watakuwapo wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi, baadhi ya wanachama, wanahabari, viongozi wa serikali, wanafamilia wa mwekezaji na kuna nafasi kama 60 hivi za marafiki wa Dewji ambao ni Wakurugenzi Watendaji wa makampuni pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa nje na ndani ya nchi,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hizo, Mulamu Nghambi.
“Kiufupi hizi ni tuzo ambazo yeye mwekezaji ameona azianzishe ili kutambua mchango wa watu mbalimbali katika mafanikio ya Simba kwenye msimu na zitakuwa endelevu. Kupitia tuzo hizi pia anaamini ataongeza hamasa kwa klabu ili iweze kupata mafanikio zaidi.
“Kimsingi Dewji na sisi kama kamati tumejipanga kuhakikisha tuzo hizi zinakuwa za kihistoria na kadiri muda utakavyozidi kwenda mbele, kutakuwa na maboresho makubwa zaidi ambayo yatazifanya zisiwe na mpinzani.”
Nghambi aliongeza kusema hakuna vigezo vilivyowekwa katika zoezi la upigaji kura na badala yake mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba watachagua washindi kwa utashi wao.
“Tumeona tuwape uhuru mashabiki kupiga kura kwa jinsi wao walivyoitazama timu katika msimu uliomalizika. Kama unavyofahamu kila mtu ana muono wake wa soka, sasa kwa kuwa wao mashabiki ni sehemu ya timu, basi nao tumeona tuwape kipaumbele katika kuendesha zoezi hili.”
Mwanaspoti

Post a Comment

Responsive Advertisement
Responsive Advertisement
Responsive Advertisement