
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba chini ya Kaimu Kocha Mkuu Masudi Djuma leo wamefanya mazoezi ya mwisho huko Nakuru kujiandaa na mchezo wa fainali michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia kesho.
Kesho Simba itakuwa na nafasi ya kuandika historia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa timu ya kwanza kucheza katika ardhi ya Uingereza ndani ya dimba la Goodison Park.
Djuma, anayeaminiwa sana na
mashabiki wa Simba, sambamba na kikosi chake wameahidi kupambana
kuhakikisha wanatwaa taji la SportPesa Super Cup kwa kuwafunga mabingwa
watetezi, Gor Mahia.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo kuelekea mchezo huo, Djuma amesema wamejipanga na
watahakikisha wanashinda mchezo huo kwa kuwa kila mmoja anatamani kwenda
Uingereza.
“Mimi na wachezaji wangu hakuna aliyewahi kufika, tunataka kwenda England,” amesema
Naye Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya Simba, Haji Manara amesema wana imani kubwa kwa kocha Djuma na kikosi chake.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Manara amewapa ujumbe maalum kocha Djuma pamoja na wachezaji wa Simba.
“Kocha
Masudi Djuma wanasimba wana imani kubwa na wewe. wanajua unao uwezo wa
kuongoza kikosi kesho kwa kushinda na timu kucheza soka bora.
“Mohammed
Hussein najua unajua thamani ya jezi ya Simba huku ukiwa na kitambaa
cha unahodha, nendeni mkapigane kesho kwa manufaa ya nchi, klabu na
maisha yenu.
“Mna dakika tisini za kutengeneza
historia kubwa ambayo haitasahaulika. Mtakuwa klabu ya kwanza EA kucheza
Goodison Park.”Tunawaamini na Tanzania inawategemea…God bless us
Post a Comment