
Jana Jumapili March 11-2018, klabu ya Azam FC, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Mbao Fc.
Mabao ya Azam FC yalufungwa kiustadi na wachezaji waliotokea benchi
kipindi cha pili, akianza winga machachari kikosini hapo Idd Kipagwile,
dakika ya 63 akimalizia kwa kichwa krosi safi ya beki wa kushoto Bruce
Kangwa.Dakika tisa baadae mshambuliaji Bernard Arthur, aliyeingia dakika ya 61 kuchukua nafasi ya Shaaban Idd, aliipatia bao la pili Azam FC kwa jitihada binafsi akimalizia pasi safi ya juu ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kabisa hivi sasa.
Mbao ilijitutumua na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 89, lililofungwa na James Msuva, mdogo wake na staa wa Tanzania, Simon Msuva, anayesakata soka la kulipwa nchini Morocco hivi sasa.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika Afisa Habari wa Simba Sc Haji Manara alimsifia mfungaji wa Bao la kwanza Idd Kipagwile kwa kiwango kizuri anachokionesha mchezaji huyo na kwenda mbali kwa kusema ingekuwa bora zaidi winga huyo akajongea Unyaman
Post a Comment